Kushuka moyo

Karibu kila mutu anashuka moyo mara kwa mara, lakini kwa wengine hisia zao ni za nguvu sana na zinaendelea zaidi.

Kushuka moyo namna hii hakuondoki kwenyewe. Kumwambia mutu ‘uchangamuke’ au ‘ujirekebishe mwenyewe’ haina mafaa. Siyo rahisi hivi.

Walakini, kuna tumaini. Kushuka moyo ni ugonjwa unaoweza kutibiwa. Daktari anaweza kuamuru mutu apate dawa au utabibu – au kuchanga yote mbili.

Jambo la muhimu ni kutafuta msaada.

Dalili za kuangaliwa:

  • Tabia ya kushuka moyo – siku nzima, siku zote
  • Tabia inayobadilikabadilika – mara moja moyo inafurahi, mara inashuka
  • Upungufu wa nguvu na ukosefu wa kupenda maisha
  • Kukasirika upesi na utukutu
  • Ukosefu wa usingizi wa kawaida – kulala mingi au kutokulala kwa kutosha
  • Kuongeza au kupunguza kilo za mwili
  • Hisia za hatia na maoni ya kwamba hana thamani
  • Kutoweza kukaza fikira au kutoweza kufikiri wazi
  • Upungufu wa kupenda kufanya ngono
  • Mawazo juu ya mauti na kuweza kuchagua kujiua

Ikiwa unajua mutu anayetaabika kwa kushuka moyo kunakoendelea:

Umtie moyo kwenda kuangalia daktari au mwenye kazi ya utabibu. Uwe tayari kupatwa naye (kwa kujua namna ya kumsaidia, piga hapa.

Do you want to contact Befrienders Worldwide?

Contact the Befrienders Worldwide member in your own country if there is one.

Find a support centre

If there are no Befrienders Worldwide members in your own country, click on the link below to find further help.

Further Support