Vionyo vya kujiua

wa kawaida, kujiua hakutokei kwa ghafula. Katika siku na saa mbele ya mutu kujiua, mara nyingi kuna vionyo na dalili.

Dalili za nguvu sana ni katika maneno – ‘Siwezi tena,’ ‘Hakuna mafaa katika maisha yangu,’ hata ‘Nadhani kwamba ni afadhali nife.’ Sikuzote ni lazima kupokea masemi ya namna hiyo kama ni ya maana.

Dalili nyingine za kawaida ni hizi:

  • Kushuka moyo au kutaka kuwa peke
  • Kujihatirisha bure
  • Kupanga vitu na kutoa vitu vyake vya bei kama zawadi
  • Kubadilika wazi kwa tabia, maoni au sura
  • Kutumia vibaya dawa za kulevya au pombe
  • Kupotewa na mutu au mali au kupatwa na mabadiliko ya maisha

Orodha hapa chini yaonyesha mifano mingine. Kila mmoja unaweza kuwa kionyo ya kwamba mutu anafikiria kujiua. Mara nyingi mambo haya hayapeleki mpaka kujiua. Walakini, ikiwa mutu anazidi kuonyesha dalili, anazidi kuelekea kujiua.

Mambo yalivyo

  • Kutendewa kwa ukatili au kutumiwa vibaya kwa ngono
  • Jeuri au kujiua imetendeka katika jamaa
  • Mauti ya rafiki au ndugu wa karibu
  • Kuvunjwa kwa ndoa au kuachana na mchumba
  • Kushindwa katika shule, majaribu yanakuja, matokeo ya majaribu
  • Kupoteza kazi, matatizo ya kazi
  • Kuwa na kesi ya karibu mahakamani
  • Kuwa katika gereza siku hizi au karibu kotoka gerezani

Mwenendo

  • Kulia machozi
  • Kupigana
  • Kuvunja sheria
  • Kufanya kwa haraka
  • Kujikata
  • Kuandika habari za mauti na kujiua
  • Alitangulia kuwa na mwenendo wa kujiua
  • Mwenendo wa kupita kadiri
  • Mwenendo unabadilika

Mabadiliko katika mwili

  • Ukosefu wa nguvu
  • Usumbufu wa namna ya usingizi – kulala mingi mno au usingizi hautoshi
  • Kupoteza tamaa ya chakula
  • Kupoteza au kuongeza kilo za mwili kwa ghafula
  • Kuongezeka kwa ugonjwa mdogo
  • Kugeuka kwa namna ya kupenda ngono
  • Namna ya kuonekana imebadilika kwa ghafula
  • Hapendezwi tena na sura yake

Mawazo na Maoni

  • Anafikiria kujiua
  • Upweke – ukosefu wa msaada kutoka kwa jamaa na rafiki
  • Kukataliwa, kuona kana kwamba ametengwa
  • Huzuni ya uzito au hisia za hatia
  • Kutokuweza kuona mambo mengi, machache tu
  • Kuota wakati angali macho
  • Wasiwasi na kukazwa
  • Kuwa hoi
  • Kujiona bure

Ikiwa unahangaikia mutu unayejua, usikose kuangalia kurasa zetu zinazoonyesha namna ya kusaidia.

Do you want to contact Befrienders Worldwide?

Contact the Befrienders Worldwide member in your own country if there is one.

Find a support centre

If there are no Befrienders Worldwide members in your own country, click on the link below to find further help.

Further Support

As proud sponsors of Befrienders, we're committed to supporting their vital work. At Vavada, we offer an unparalleled gaming experience with top-notch security, generous bonuses, and a wide variety of games to suit every taste. Join us and enjoy the benefits that come with our partnership, bringing both excitement and reliability to your entertainment.