Kuhusu vituo vya Befrienders Worldwide

Vituo vya Befrienders Worldwide hutoa huduma ya siri ya kihisia kwa mtu yeyote aliye katika mtanziko.

Vituo vyetu

Lengo kuu la vituo hivyo ni kutoa huduma ya kihisia kwa watu wenye mawazo ya kujitia kitanzi.. Vituo hivyo pia hupunguza masaibu, upweke, kukata tamaa na unyogovu kwa kumsikiliza mtu yeyote ambaye anahisi hana mahali pa kuegemea..

Vituo vya Befrienders vinaendeshwa na watu waliojitolea ambao wamepewa mafunzo maalum. Kazi hiyo sio ya kisiasa wala kidini, nao waliojitolea hawawezi kulazimisha maoni yao kwa mtu yeyote. Wao usikiliza tu.

Ingawa mtu amekuwa akiwasiliana na kituo iwe kwenye simu,barua pepe, gumzo kwenye mtandao, ujumbe wa maandishi SMS au kwenye mkutano wa ana kwa ana ni siri ,atakile atakacho mweleza muhudumu wa Befrienders. Baadhi ya wale wanaopiga simu hupendelea kutojitambulisha kwa majina, na hiyo ni sawa.

Je! Unataka kuwasiliana Befrienders Worldwide?

Wasiliana na Mwanachama Befrienders Worldwide katika nchi yako ikiwa kuna moja.

Pata kituo cha msaada

Ikiwa hakuna washiriki Befrienders Worldwide katika nchi yako mwenyewe, bonyeza kwenye kiunga hapa chini kupata msaada zaidi.

Msaada zaidi