Mtu wa kusikiliza
Mtu ambaye atachukuwa muda ili kuwasikiliza kwa uhakika
Mtu ambaye hatahukumu, au kutoa ushauri au maoni, lakini atatoa makini yasiyogawanyika
Mtu wa kumwamini
Mtu atakaye waheshimu na hatajaribu kuchukuwa usukani .
Mtu ambaye atachukulia kila kitu kwa usiri mkuu
Mtu wa kujali
Mtu ambaye atapatikana, kumweka mtu kwa raha bila wasiwasi na kuzungumza kwa upole
Mtu ambaye atamhakikishia tena, atakubali na kuamini. Mtu ambaye atasema, “Ninajali.” “
Mtu ambaye anaweza kuzungumzia wazi kuhusu kujitoa uhai
Mtu wa kuzungumza naye kuhusu mawazo ya kujitoa uhai na hupangilia bila kuwa wa kuhukumu
Mtu wa kusaidia kufikiria njia nyinginezo za kukabiliana na matatizo sasa na mbeleni
Mtu ambaye anahimiza kufikiria kuhusu machaguo tofauti ya kukabiliana vyema na ugumu wowote