Hamna njia rahisi ya kuja kufarijika kutokana na kupotewa na mpendwa ambaye alifariki kwa njia ya kujiua. Hapa chini kuna maelezo ambayo tunaamini yatasaidia kupunguza majonzi ya msiba. Kuna njia nyingine ambazo huenda zikawa na manufaa kwako wewe katika Msaada na Ufadhili.

Tafadhali chagua sehemu moja hapa chini:

Miitiko na Hisia

Mahitaji

Msaada na Ufadhili

Miitiko na hisia

Chanzo cha msaada

Vituo vya Urafiki (Befrienders centres) hutoa ufadhili wa hisia kwa faragha kwa mtu yeyote anayepatwa na mzozo.

Kupotewa na mtu wa karibu yako, huleta majonzi mengi na kuomboleza. Kupotewa na mtu kwa njia ya kujiua mwenyewe mara nyingi hupelekea kuwa na huzuni na maombolezo makubwa zaidi. Kupotewa na mtu kwa njia ya kujiua mwenyewe husababisha hali na hisia mbali-mbali. Msiba kutokana na mtu aliyejiua hurefuka. Mshituko, utengano wa kijamii na kujisikia kuwa na hatia mara nyingi huwa mkubwa zaidi na nafasi ya kupata kuchagua husababisha maswali ya kuumiza.

Huenda ukakutana na baadhi ya haya yafuatayo:

Mshtuko Mkubwa

Hisia ya mshtuko na kutoamini kufuatia kifo cha aina hii huenda ikawa kubwa. Jambo la kawaida kuhusiana na msiba kama huu ni kutokewa na maono mbali-mbali ya jinsi kifo hicho kilivyotukia, hata ikiwa kifo hicho hakikushuhudiwa. Kupata mwili nako pia kwaweza kuwa kiwewe kingine na kisa kisichoelezeka. Ni haja ya kawaida kwa mtu kurejelea mara kwa mara maono haya ya kuogofya na kuumiza juu ya kifo hicho na hisia yanayoweza kutengeneza.

Kujiuliza - Kwa nini?

Mfiwa wa mtu aliyefariki kwa njia ya kujiua mara nyingi husababisha utafiti wa muda mrefu wa ufafanuzi juu ya mkasa huo. Watu wengi kasha huja kukubali kwamba kwa kweli hawataweza kujua sababu kamili. Wakati wa utafiti wa maelezo, watu mbali-mbali wa jamaa hiyo huenda wakawa na maoni yanayotofautiana juu ya sababu ya kifo kama hicho kilivyotukia. Hali hii yaweza kuleta farakano ya uhusiano miongoni mwa jamaa, hasa ikiwa kuna dalili za kuweka lawama.

Kujiuliza - Ingeliweza kuepukika?

Ni kawaida kabisa kurejea mara nyingi kwa kuwaza jinsi kifo hicho kingelivyoweza kuzuiwa na jinsi mpendwa huyo angelivyoweza kuokolewa. Kila kitu chaweza kuonekana kuwa cha kuumiza kwa mtazamo. Mawazo ya ‘Jee ingelikuwa' yaweza kuonekana kana kwamba hayataisha. Kurudia kufikiria matukio ni njia ya kawaida nay a lazima kwa kuweza kukabiliana na kile kilicho tukia. Utafiti umeonyesha kwamba baadhi ya wafiwa wa watu waliojiua hujisikia kuwa na hatia, kujilaumu na kujiuliza kila mara kuliko wafiwa wa aina nyingine za kifo.

Kuwachwa/Kukataliwa

Waweza kujisikia kana kwamba umekataliwa. Ni kawaida kujisikia umewachwa na mtu ambaye ‘anachagua' kufa.

"Mimi nilichukiwa na kwamba hakuja kuongea nasi. Nafikiri sote tulipata kukasirika wakati mmoja au mwengine. Wewe unafikiria: ‘Ilikuwaje kutufanyia jambo kama hili?'" Dada ambaye kaka yake alijiua. .

Hofu ya kujiua na hisia

Kukata tama ni sehemu moja ya kawaida ya kuomboleza , lakini baada ya kifo cha mtu wa karibu aliyejiua kukosa tumaini huenda ikacganganyika na hofu ya usalama wako mwenyewe. Kujitambulisha na mtu ambaye amejiua kwaweza kuwa tishio kubwa la hisia zako za usalama. Unaweza kukabiliwa na wasiwasi mkubwa zaidi kuliko wale ambao ni wafiwa kwa njia nyingine za kifo na hata kuwa na hatari ya kupata hisia za kutaka kujiua pia.

Kuvutia Vyombo vya Habari

Wakati mtu anafariki kutokana na njia ya kujiua au hali nyingine ambazo hazikutarajiwa , huenda ikavutia jamii. Uchunguzi ambao huenda ukahitajika kisheria hulenga mtu yule aliyefariki na pia kwa jamaa wake wa karibu na marafiki zake. Kujulikana kwa haraka na vyombo vya habari, kwaweza kusababisha huzuni kali zaidi kwa jamaa waliofiwa na marafiki, hasa pale kifo kama hicho kinaripotiwa kwa njia ya kutojali au bila usahihi.

Fedheha na Upweke

Tabia za kijamii katika swala hili la kujiua zinabadilika, lakini huenda zikaendelea kupunguza ufadhili uliopo sasa. Unyamavu wa wengine waweza kuongeza nguvu za kupatwa na huzuni, aibu na ‘kuwa tofauti'. Ikiwa wengine wanaona haya, dukuduku au kuepaepa swala la kujiua, huenda ukawachwa katika hali ya kujisikia na upweke mkubwa.

Nafasi ya kuongea, kukumbuka na kusherehekea aina zote za maiasha ya mpendwa na umaarufu huenda ukaunyimwa. Haja kubwa ya kulinda mpendwa na wewe mwenyewe kutokana na kuhukumiwa na wengine pia kwaweza kujitokeza.

Mama mmoja aliyekuwa akiandika juu ya kifo cha mwanawe wa kiume alisema kwamba hatujawahi kuambiwa la kusema ikiwa tunaongea juu ya kifo cha mmoja wetu katika jamaa ambaye amejiua. Alihitaji kuambiwa kitu kicho hicho ambacho chaweza kutamkwa kwa mtu mwengine ambaye alipatwa na kifo cha mtu wa karibu naye: "Nasikitika mno kwa huzuni kubwa iliyokupata na kuna chochote ninachoweza kufanya? Ikiwa ungelitaka kuongea juu yake, mimi ni msikizi. Angalau nina pahali pa kujiliwaza."

© The Royal College of Psychiatrists 1997
Imechukuliwa kutoka kwa Kijitabu cha Maelezo ya Ufiwa kilichoandikwa na Kate Hill, Keith Hawton, Aslog Malmberg na Sue Simkin
Kimechapishwa upya kwa ruhusa ya The Royal College of Psychiatrists

Mahitaji

Kundi moja la watu kutoka nchini Canada waliofiwa na watu waliojiua walishauriwa na wakajisikia kwamba walihitaji msaada na ufadhili kwa:

 • kuileta hali ya kujiua katika taswira
 • kukabiliana na matatizo ya jamaa yaliyotokana na kifo cha kujiua
 • kujisikia nafuu wao wenyewe
 • kuongea juu ya kifo cha kujiua
 • kupata maelezo ya visa vya kujiua na madhara yake
 • kupata pahali salama pa kutoa mawazo yao have
 • kuelewa na kukabiliana na maoni ya wengine juu ya visa vya kujiua
 • kupata ushauri juu ya maslahi ya utendaji/ujamii

© The Royal College of Psychiatrists 1997
Imechukuliwa kutoka kwa Kijitabu cha Maelezo ya Ufiwa kilichoandikwa na Kate Hill, Keith Hawton, Aslog Malmberg na Sue Simkin
Kimechapishwa upya kwa ruhusa ya The Royal College of Psychiatrists

Msaada na Ufadhili

Lini utafika wakati wa kupata usaidizi?

Huzuni yaumiza na kuchosha. Siyo rahisi kila mara kuamua ni lini utakuwa wakati mzuri wa kupata usaidizi. Huenda ukachagua kutafuta usaidizi ikiwa wewe:

 • unaendelea kujisikia na ganzi na utupu miezi kadhaa baada ya kufiwa
 • huwezi kulala au unaptwa na jinamizi
 • unajisikia huwezi kumudu hisia ngumu au mhemko wa mwili kama vile uchovu, kuchanganyikiwa, wasiwasi, hamaki au fadhaa sugu
 • kujisikia umeshindwa kabisa na mawazo na hisia kutokana na kifo cha mpendwa wako k.m. hasira, hatia, kukataliwa kusikia kuna haja ya kushirikiana na mwengine juu ya hali yako lakini hamna mtu yeyote wa kufanya hivyo.
 • Kujiweka hali ya kuchangamka ili usijisikie (k.m. kufanya kazi wakati wote)
 • Unajikuta umekuwa ukitumia madawa ya kulevya kupita kiasi
 • Kujikuta una wasiwasi na kufikiria juu ya kujiua hata wewe mwenyewe
 • Kuwa na hofu kwamba wale walioko pamoja nawe wanaweza kupatwa na hali hiyo ya kujiua na wasiweze kuimudu

Baadhi ya sehemu za ufadhili na jinsi zinavyoweza kukusaidia:-

Makundi ya Kujisaidia-wenyewe

Hukuwezesha wewe na wengine kukutana na kubadilishana mawazo na mambo mliyo pitia na huenda hali hii ikakupa uhakikisho tena

Madaktari wa Mtaani

 • wanaweza kusikiliza, kuzungumza na kutoa usaidizi wa kihisia
 • wanaweza kukusaidia na matatizo kama ya kukosa usingizi, wasiwasi au huzuni
 • wanaweza kukushauri juu ya pahali pengine pa kupata usaidizi.

Ufadhili utakuwa tofauti kutoka kwa daktari mmoja hadi daktari mwengine. Haiwezekani kwa wewe kuongea juu ya kila kitu kilichotukia katika mihadi mifupi. Ili kuweza kuepukana na hali hiyo, unaweza kumuandikia Daktari kabla ya mihadi yako kufika.

Kushauri

 • hutoa muda zaidi wa kuongea mambo yote au ufadhili wa muda mrefu zaidi
 • hakukulazimishi wewe kuegemea yaliyopita lakini badala yake hukupa msaada wa kukabiliana na mzozo wa kihisia na mabadiliko ya maisha ambayo huenda unapitia.
 • Hukupuimzisha kwa ambavyo kukupa nafasi ya kuongea na mtu mwengine ambaye ni mgeni kwako na katika mazingara ya salama.

Dini:

 • Yaweza kuwa chanzo cha kukupa nguvu na ufadhili ikiwa wewe ni mtu unayezingatia imani za kidini.
 • Viongozi wa kidini katika mtaa wako huenda wakawa chanzo cha ufadhili unaoweza kutegemea.

Vituo vya Urafiki

Hutoa usaidizi wa faragha kwa mtu yeyote ambaye ana huzuni au kutapatapa au ambaye anapitia hali ya hisia za kujiua. Kupata pahali pa usaidizi karibu nawe bonyeza hapa.

Mashirika Maalumu ya Ufiwa

Baadhi ya mashirika ya Ufiwa yameorodheshwa katika miunganisho ifuatayo:-

Chama cha Kimataifa cha kuzuia hisia za kujiua
www.med.uio.no/iasp/english/cs.html

Chama cha Amerika cha elimu ya hisia ya kujiua
www.suicidology.org/displaycommon.cfm?an=6

Chama c ha Canada kwa kuzuia hisia za kujiua
www.casp-acps.ca

Mashirika ya Uingereza


Orodha kamili ya mashirika ya ufiwa, na Vitabu vya kufaa, inaonyeshwa kikamilifu katika Kijitabu cha maelezo cha Royal College of Psychiatrists. Unaweza kufungua pdf ya kijitabu hicho hapa.

© The Royal College of Psychiatrists 1997
Imechukuliwa kutoka kwa Kijitabu cha Maelezo ya Ufiwa kilichoandikwa na Kate Hill, Keith Hawton, Aslog Malmberg na Sue Simkin
Kimechapishwa upya kwa ruhusa ya The Royal College of Psychiatrists